0
Timu ya Hispania imezindua jezi zake ambazo itazitumia kwenye michuano ya Ulaya ya mwaka 2016  nchini Ufaransa.


La Roja, ambao walishinda kombe hilo mnamo mwaka 2008 na 2012 wamebadilisha aina yao ya jezi za asili kwa kuuhamishia ufito wa rangi ya njano ubavuni mwa jezi na kaptula zao badala ya mabegani kama ilivozoeleka.


Jezi hiyo mpya ya timu ya Hispani imezinduliwa kwa pamoja na wachezaji wote wa kikosi cha timu hiyo lakini pia mlinzi wa Barcelona Jordi Alba, Kiungo wa klabu ya Manchester City David Silva, mlinda mlango wa klabu ya Porto Iker Casillas, kiungo mchezeshaji wa Atletico Madrid Koke na  mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa walikua na picha tofauti kutokana na udhamini wao binafsi wa kampuni ya Adidas.




Post a Comment

 
Top