0
MABINGWA wa Ligi ya mabingwa barani Ulaya, Real Madrid ya nchini Hispania jana wameinyuka Sevilla wanaoshikilia taji la Europa  mabao 3-2 na kunyakua ubingwa wa Super Cup.

Kipindi cha kwanza kilimalizika kwa timu hizo kwenda mapumziko zikiwa zimetoshana nguvu kwa bao 1-1 huku Sevilla ikitawala zaidi mchezo ambao Madrid iliwakosa nyota wake kadhaa akiwemo Cristiano Ronaldo, Pepe, Gareth Bale na Toni Kroos.

Madrid ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 21 kupitia kwa kinda Marco Asensio aliyeachia shuti kali akiwa nje ya 18 lakini Franco Vasques akaisawazishia Sevilla dakika 41.

Kipindi cha pili cha mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Larkendal nchini Norway kilianza kwa kasi huku Sevilla wakionekana kuliandama zaidi lango la Madrid.

Konoplyanka aliipatia Sevilla goli la pili kwa mkwaju wa penati baada ya Sergio Ramos kufanya madhambi kwenye eneo la hatari.

Baada ya bao hilo Madrid waliliandama lango la Sevilla kama nyuki lakini ukuta wa mabingwa hao wa Europa ulikuwa imara kuondosha hatari zote hadi dakika 90 za mtanange huo zilipomalizika ndipo katika dakika tatu za nyongeza Ramos akaisawazishia Madrid.

Mechi hiyo ilikwenda katika muda wa nyongeza wa dakika 30 ambapo katika dakika ya 28, Danny Carvajal aliipatia Madrid bao la tatu na la ushindi hivyo kutawazwa kuwa mabingwa wa kombe hilo.
TATHIMINI YA MCHEZAO.
 

REAL MADRID: Casilla, Carvajal, Varane, Sergio Ramos, Marcelo, Kovacic (James 72), Casemiro, Isco (Modric 66), Lucas, Morata (Benzema 62), Asensio

Wasiotumika: Yanez, Nacho, Danilo, Llorente

Wafungaji: Asensio 21, Ramos 90+3, Carvajal 119 

Kadi za njano: Carvajal, Asensio, James

SEVILLA: Sergio Rico, Pareja, Kolodziejczak, Carrico (Rami 51), Kiyotake, Iborra (Kranevitter 74), Vazquez, Nzonzi, Mariano, Vietto (Konoplyanka 67), Vitolo

Wasiotumika: Soria, Ben Yedder, Sarabia, Escudero

Wafungaji: Vazquez 41, Konoplyanka 72

Kadi za njano: Vitolo, Kolodziejczak

Kadi nyekundu: Kolodziejczak 93

Mwamuzi: Milorad Mazic (Serbia)




Post a Comment

 
Top