1
Timu ya Vital’O ya Burundi imetuma jina la mshambuliaji Laudit Mavugo kwenye usajili wake wa msimu ujao wa ligi ya Burundi kama sehemu ya mchezaji wao.

Uongozi wa Vital’O kupitia kwenye mtandao wao umesisitiza kuwa Mavugo bado ni mchezaji wake na inashangazwa kusikia amesajiliwa na Simba bila wao kufahamu.

“Tunachojua amekwenda kufanya majaribio Ufaransa kwa ruhusa yetu sasa tunashangaa kusikia yuko Tanzania na amesajiliwa na Simba,” imesema taarifa hiyo.

Simba tayari imemsaini Mavugo kwa mkataba wa miaka miwili na haijajulikana kwamba wamemalizana vipi na Vital’O ambayo ndiyo inammiliki mshambuliaji huyo aliyeanza vizuri kibarua chake kwa kufunda bao katika mechi ya kwanza ya kirafiki dhidi ya AFC Leopard ya Kenya.

Laudit Mavugo raia wa Burundi amewatoa hofu mashabiki wa Simba ambao wamekuwa na wasiwasi kwamba huenda atashindwa kuichezea timu hiyo baada ya kuwepo taarifa kuwa ana mkataba wa mwaka mmoja na timu yake ya zamani ya Vital'O. 

Mavugo amedai kuwa hana mkataba na Vital'O ila kitu pekee anachowaomba viongozi wa Simba ni kwenda kumalizana haraka na timu yake iliyomkuza kisoka ya Solidarite ambayo ndiyo yenye mamlaka ya kutoa ITC yake. 

Mavugo alisema kuwa siku 20 zilizobaki ni chache hivyo ni vyema kukamilisha jambo hilo haraka ili lisimzuie kukipiga Msimbazi msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

Post a Comment

  1. Best Baccarat | Play & Win Online | No Limit Casino
    › gambling › baccarat choegocasino › gambling › baccarat 바카라사이트 Find the best casino and online poker sites that provide baccarat, plus the best casino games. Learn about playing 제왕카지노 at online baccarat with real money.

    ReplyDelete

 
Top