0
KIINGILIO cha cnini katika mchezo wa marudiano Kundi A kombe la Shirikisho kati ya wenyeji, Yanga SC na Mo bejaia kitakuwa Sh 3,000 kwa majukwaa ya mzungunguko.
 
Taarifa ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imesema kwamba viti vya kijani, bluu na chungwa wakati Viti Maalumu vyenye hadhi ya daraja B na C kiingilio kitakuwa Sh 10,000 wakati A kiingilio kitakuwa ni Sh 15,000 kwa mujibu wa Waratibu wa Young Africans.
 
Kikosi cha watu 35 ambao ni wachezaji na viongozi wa MO Bajaia kutoka Algeria, wametua Dar es Salaam, usiku wa kuamkia jana Agosti 9, 2016 na imefikia Hoteli ya Ledger Plaza, iliyoko Kunduchi Beach nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Timu hiyo imekuja kucheza na Young Africans ya Dar es Salaam, katika mchezo wa nne wa hatua ya Nane Bora kuwania Kombe la Shirikisho Barani Afrika utakaofanyika Jumamosi Agosti 13, 2016 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Licha ya kwamba Young Africans kuwa na pointi moja, bado ina nafasi ya kushika nafasi za juu katika kundi la A ambalo msimamo wake unaongozwa na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), huku Mo Bajaia ya Algeria na Medeama ya Ghana, zina pointi tano kila moja.

Wakati Young Africans wanacheza na Mo Bajaia iliyoshinda mchezo wa kwanza huko Algeria, Medeama itakipiga na TP Mazembe.

Mchezo wa Young Africans dhidi ya Mo Bajaia utachezeshwa na waamuzi kutoka Ethiopia ambako katikati atakuwa Bamlak Tessema Weyesa akisaidiwa na Kindie Mussie mstari upande wa kusini na Temesgin Samuel Atango katika mstari wa Kaskazini upande wa wakati Mwamuzi wa Akiba atakuwa Haileyesus Bezezew Belete.

Kamishna wa mchezo atakuwa Gaspard Kayijuka kutoka Rwanda wakati Desire Gahuka wa Burundi atasimamia ufanisi wa waamuzi wa mchezo na Mratibu Mkuu wa mchezo atakuwa Isam Shaaban kutoka Sudan.

Mratibu huyo anatarajiwa kuwasili leo Agosti 10, 2016 wakati waamuzi watatua kesho Agosti 11, 2016 na msimamizi wa waamuzi atatua Ijumaa Agosti 12, 2016.

Post a Comment

 
Top