0
NAHODHA John Raphael Bocco ‘Adebayor’ jana usiku ameinusuru Azam FC kulala mbele ya URA ya Uganda baada ya kuisawazishia bao mwishoni mwa kipindi cha pili katika sare ya 1-1 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Bocco aliifungia Azam FC bao la kusawazisha dakika ya 73 kwa penalti baada ya mchezaji aliye katika majaribio kutoka Zimbabwe, Francesco Zekumbawire kuchezewa rafu na Julius Ntambi kwenye eneo la hatari.

Wakusanya Kodi wa Uganda, URA walipata bao la kuongoza mapema tu baada ya kuanza kipindi cha pli kupitia kwa Labama Bakota aliyefunga kwa kichwa akimalizia krosi ya Shafiq Kagimu.

URA wanatarajiwa kucheza mechi yao ya pili katika ziara yao ya Tanzania Jumapili, watakapomenyana na Simba SC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kikosi cha Azam kilikuwa:Aishi Manula, Bruce Kangwa, Shomari Kapombe/Ismail Gambo dk 46, Jean Mugiraneza, David Mwantika, Himid Mao, Masoud Abdallah/Bolou dk 46/Mcha dk 75, Frank Domayo/Mudathir dk 46, Salum Abubakar/Singano dk 63, Shaaban Idd/Bocco dk 46 na Gonazo Bi Thomas/ Zekumbawire dk 46

URA FC: Muwanga Mathias, Ntambi Julius, Sekitto Samuel/Munaaba Allan dk 87, Kawooya Fahad, Kulaba Jimmy, Agaba Oscar, Kagimu Shafik/Kagaba Nicholas dk 71, Lwasa Peter/Elkanah Nkugwa dk 55, Feni Ali/Wandyaka Richard dk 82, Bokota Labama, Lule Jimmy

Post a Comment

 
Top