0
Na Onesmo Emeran.
LIGI Maarufu Songea Mjini eneo la bombambili katika uwanja wa Sokoine "Sangaone Cup" inatarajia kuanza kutimua vumbi mapema mwezi huu tarehe 21 siku moja baada ya ligi kuu ya Tanzania bara pia kuanza kutimua vumbi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kamati ya usimamizi wa ligi hiyo mapema jana mdhamini mkuu wa ligi ambaye pia ni diwani wa kata ya Bombambili Golden Sanga maarufu "Sangaone" amesema ligi hiyo safari hii imeboreshwa kwa kiasi fulani ukifananisha na ligi msimu uliopita kwa upande wa zawadi.

"Pamoja na uchumi kuwa mgumu, Sangaone Cup haijarudi nyuma kwa upande wa zawadi, na safari hii imeboresha kwa kiwango fulani,Mshindi Wa kwanza ataibuka na fedha taslimu shillingi laki tatu (300,000/=) na Kombe,Mshindi wa pili atapata shilingi laki mbili(200,000/=)na Kombe,na Mshindi wa tatu atapata Laki moja(100,000/=)na Mpira.
 
Lakini pia kutakuwa na timu yenye nidhamu ambayo itapata Mpira,Mfungaji bora atapata shillingi elfu hamsini(50,000/=)".Alisema Sangaone.

Aidha mdhamini huyo mkuu amewaomba radhi wakazi wa Mjini Songea ambao wamekuwa wakifuatilia mashindano hayo kuwa  yamechelewa kidogo kuanza kama ilivyo kawaida huanza mapema mwezi may na hii ni sababu ya mashindano mbalimbali ambayo yamechukua nafasi kwa kipindi chote cha kuanzia mwezi may mpaka hivi sasa.

Na katika hatua nyingine Sangaone amevitaka vilabu vyote kufuata taratibu pindi wanapoona wameonewa na hasa watu wa bomba mbili kufuata utaratibu pale wanapoona hawajatendewa haki kuliko kutoa magoli kama njia ya kupata haki yao.

Post a Comment

 
Top