0
TAARIFA KWA UMMA

Klabu ya Simba kwa furaha iliyochanganika na huzuni kubwa,kesho inatarajiwa kumuaga LEGENDARY wake Mussa Hassan'Mgosi' kwenye mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Timu ya URA ya nchini Uganda,
Mchezo utakaonza saa kumi alasiri katika uwanja wa Taifa uliopo jijini Dar es salaam

Mgosi aliyeitumikia klabu yetu kwa mafanikio na nidhamu kubwa ameamua kustaafu kucheza soka ya ushindani na kuwaachia vijana,ataagwa kwa heshima zote kama mchezaji aliyeacha alama kubwa 'LEGACY' kwenye klabu yetu.

Kwa nidhamu aliyoionyesha na mapenzi yake kwa klabu.Simba imeamua kuendelea kumtumia kama meneja wa timu kuanzia kesho,mara baada ya kustaafu rasmi.
 
Huku Abbas Alli akiwa mratibu wa timu atakaeshirikiana na Mgosi kwenye usimamizi wa masuala ya timu kwa ujumla.

Nitumie fursa hii kuwaomba sana wana Simba tujitokeze kwa wingi kwenye mchezo huo muhimu na maalum ili muweze kuona kikosi chenu kwa mara ya mwisho,kabla ya kuanza kwa ligi kuu ya Vodacom mwishoni mwa wiki ijayo.

Kwa sasa timu ipo kambini na kocha wetu Joseph Omog ameahidi kushusha 'mashine'zake ili sio tu kuwafunga URA.bali pia kuonyesha soka safi itakayoburudisha kama ilivyo falsafa ya kudumu ya timu ya Simba.

Halikadhalika klabu inawashukuru klabu ya Azam ambao tumeshirikiana nao kuileta timu hii ya Uganda ambayo imeonyesha uwezo mkubwa kwenye mechi yao dhidi ya vijana kutoka Chamanzi.

Niwaarifu pia kesho kutakuwa na udhibiti mkubwa wa uingiaji mpirani,sambamba na udhibiti wa walanguzi wa tiketi ambazo zitauzwa kwa kiingilio cha Shilingi 20,000 kwa VIP A.Elfu 15,000 kwa VIP B na C,na shilingi 5,000 kwa mzunguko.

Mwisho niwajulishe ulinzi na usalama kwenye mchezo huo utakuwa ni kiwango cha juu..walanguzi na wauzaji tiketi feki wajihadhari..hakutakuwa na msalie Mtume kesho.klabu haitajali cheo wala umaarufu wa mtu.
 
Matarajio yetu kila mtu atajidhibiti mwenyew kuhakikisha mapato halali yanapatikana na usalama unakuwa wa kutosha ndani na nje ya uwanja.

Nb.tumejitahidi kuweka muda mzuri zaidi ili kuwawezesha watazamaji wawahi mechi za ligi kuu ya Uingereza zinazotarajiwa kuchezwa kesho.

Imetolewa na
HAJI S MANARA
MKUU WA HABARI
SIMBA SC

SIMBA NGUVU MOJA

Post a Comment

 
Top