Tatizo la ulinzi ndani ya klabu ya Arsenal limeongezeka mara baada ya matabibu wa klabu hiyo kuthibitisha kuwa mlinzi raia wa Ufaransa Mathieu Debuchy
kuthibitika kuwa atakua nje ya uwanja kwa takribani miezi mitatu na hivyo kuikosa michezo dhidi ya Chelsea, Liverpool na Manchester
United katika kipindi hicho cha miezi mitatu atakachokuwa nje ya uwanja.
Mchezaji huyu wa kimataifa wa Ufaransa aliumia siku timu yake ilipokuwa ikicheza dhidi ya klabu ya Manchester City mchezo ambao ulimalizika kwa sare ya jumla ya magoli mawili kwa mawili Debuchy aliyenunuliwa kwa paundi milioni 12 kutoka klabu ya Newcastle amefanyiwa upasuaji siku ya ijumaa, upasuaji ambao utamlazimu kukaa nje ya uwanja kwa takribani miezi mitatu.
Michezo ambayo Debuchy atazikosa:
Arsenal vs Southampton
Arsenal vs Tottenham
Arsenal vs Galatasaray
Chelsea vs Arsenal Sun
Arsenal vs Hull
Anderlecht vs Arsenal
Sunderland vs Arsenal
Arsenal vs Burnley
Arsenal vs Anderlecht
Swansea vs Arsenal
Arsenal vs Man Utd
Arsenal vs Borussia Dortmund
West Brom vs Arsenal
Arsenal vs Southampton
Stoke vs Arsenal
Galatasaray vs Arsenal
Arsenal vs Newcastle
Liverpool vs Arsenal
Post a Comment