Louis van
Gaal amesema kuwa anatamani sana kumuona Cristiano Ronaldo akirejea ndani ya klabu ya Manchester United lakini hafikirii kama klabu ya Real Madrid itakua iko tayari kumruhusu nyota huyo kuihama klabu hiyo.
Ronaldo
aliyewahi kuyatumikia mashetani hayo ya Old Trafford kabla hajahamia Bernabeu kwa ada ya rekodi ya uhamisho wa Dunia ya paundi milioni 80 mnamo mwaka 2009.
Mchezaji huyu bora wa Dunia wa sasa anaweza kuihama klabu hiyo iwapo tu klabu inayomtaka itafikia ada sawa na hiyo iliyomng'oa yeye pale Traford.
Siku za hivi karibuni Ronaldo amekua akihusishwa sana kurejea kwenye Premier League taarifa ambazo zimekua hazifurahiwi na Magalactico hao ambao tayari mpaka sasa wameshawaruhusu wachezaji wao wakubwa kadhaa kuondoka kwenye majira haya ya joto ya usajiri.
Alipoulizwa na waandishi wa habari kama atamrejesha Ronaldo,Van Gaal alisema: ‘Kama itawezekana,
Unakumbuka nilivyosema kuhusu Falcao?, Mchezaji kama Ronaldo huwa analeta kitu cha ziada kikosini lakini sidhani kama Madrid wanaweza kumruhusu kuondoka ndani ya kikosi chao"
Post a Comment