Hamu ya klabu ya Manchester
City kumsajili mshambuliaji Radamel Falcao imeongezeka mara baada ya mshambuliaji wa timu hiyo Alvaro Negredo siku ya jana kukubali kujiunga na klabu ya Valencia.
Mabingwa hao wa
Premier League wametuma ofa kwa klabu ya Monaco yenye nia ya kumjumuisha mshambuliaji huyo kabla ya dirisha la usajiri kufungwa leo saa sita za usiku.
Alvaro Negredo amekubali kurejea nchini Spain.
Klabu ya Arsenal nayo imejiingiza katika kuicheza ngoma hiyo ya kumwania mshabuliaji huyo ili kuja kuziba pengo la mshambuliaji wake Olivier Giroud anayetarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa takriban miezi mitatu kwa kuuguza majeraha ya mguu.
Manchester
United nayo pia ilipewa nafasi ya kumsajili mshambuliaji huyo raia wa Colombia lakini haikuonesha nia ya kutaka kumsajili mshambuliaji huyo na badara yake ikamsajili mshambuliaji raia wa Argentina Angel di Maria wiki iliyopita.
Post a Comment