0
Luke Shaw (third right) looks disappointed on the Manchester United bench as his team lose 5-3 to Leicester 
Mapungufu ya klabu ya Manchester United katika sehemu ya ulinzi yalijionesha siku ya Jumapili ya wiki hii kwenye mchezo dhidi ya timu iliyopanda daraja msimu huu Leicester City wakati ambapo meneja Louis van Gaal ameendelea kuwa na wakati na mwanzo mgumu sana ndani ya kikosi cha mashetani wekundu.

Klabu hiyo imemjumuisha kikosini Muarjentina Marcos Rojo ambaye kwenye mchezo huo anaonekana hakuwa katika kiwango bora katika mchezo huo. Ili kulitatua tatizo linalo wakabili kwa sasa Manchester United itawalazimu kuwajumuisha kikosini mmoja au wawili kati ya wachezaji wafuatao ili kukiimarisha kikosi chao.

1. MATEO MUSACCHIO.

 Mateo Musacchio of Villarreal tries to keep Lionel Messi at bay during an early season meeting with BarcelonaMateo Musacchio wa Villarreal (kulia) akipambana na Lionel Messi kwenye mchezo dhidi ya Barcelona.

Mlinzi huyu wa kati wa klabu ya Villarreal amekua akiwindwa na klabu ya Manchester United kwa muda mrefu na tatizo lililokua likiwafanya United wasite kumjumuisha kikosini mlinzi huyu ni shaka waliyokua nayo juu ya urefu wake kama kweli ulikua umefikia futi 6 na nchi 1. Klabu ya Tottenham ilionesha nia ya dhahiri ya kutaka kumnunua mlinzi huyu lakini tatizo lililowakwamisha ni kushindwa kumalizana na mmiliki wa tatu wa mchezaji huyo na hivyo kumfanya abakie sokoni.

2. MATS HUMMELS.

 Borussia Dortmund defender Mats Hummels shields the ball from Bayern Munich's Arjen Robben
Borussia Dortmund defender Mats Hummels shields the ball from Bayern Munich's Arjen Robben

Klabu ya Borussia Dortmund imekataa katakata kumuuza mchezaji huyo kwa timu yoyote ile Duniani, lakini ushawishi mkubwa wa klabu ya Manchester United unaoambatana na matumizi makubwa ta pesa unaweza ukafanya mpango wa klabu hiyo utimie.

3. FABIAN SCHAR.
 Fabian Schar in action for Basle in last week's Champions League match with Real Madrid in the Bernabeu
Fabian Schar akiitumikia klabu yake ya Basle kwenye michuano ya Uefa Champions League dhidi ya Real Madrid.

Mlinzi wa klabu ya Basle ni mjanja sana kwenye kuicheza mipira ya aina zote kitu ambacho Mholanzi Louis van Gaal amekua akikipenda na kukihitaji kutoka kwa walinzi wake. Vilabu vya Premier League vya Tottenham na Arsenal vinamuhitaji sana mlinzi huyu halikadhalika klabu ya Borusia Dortmund inayomtazama mlinzi huyo kama mrithi wa Mats Hummels pindi atakapoondoka.
4. AYMERIC LAPORTE. 
Aymeric Laporte (right) in action for Athletic Bilbao against Barcelona in La Liga last weekend
Aymeric Laporte (kulia) akipambana kwenye mchezo dhidi ya Barcelona kwenye michuano ya La Liga wikiendi iliyopita.

Mlinzi wa kati Mfaransa mwenye umri wa miaka 20 anayekipiga kwenya klabu ya Athletic Bilbao na tayari ada ya uvunjaji wa mkataba wake imekwisha anikwa hadharani kuwa ni Paundi milioni 21kwa klabu itakayomtaka.
Barcelona wanamhitaji kwa udi na uvumba mlinzi huyu lakini pia mlinzi wa klabu ya Real Sociedad Inigo Martinez, mwenye umri wa miaka 23, anaonekana pia anaweza kuwa ni suluhisho kwa Barcelona na Manchester United ili kutibu matatizo yao.
5. MARQUINHOS.
Marquinhos has impressed for Paris Saint-Germain (second left) and is an accomplished centre-half
Kitendo cha klabu ya PSG kumsajili Mbrazil David Luiz kimemfanya Marquinhos kukalia kuti kavu ndani ya klabu hiyo. Hali hiyo inawafungulia milango klabu ya Manchester United kumsajili mlinzi huyo ili kwenda kuimarisha sehemu ya ulinzi ya klabu hiyo.

Post a Comment

 
Top