0
Van Gaal & Woodward to thrash out Manchester United's January transfer plansMeneja wa klabu ya Manchester United Luis van Gaal anatarajiwa kukutana na makamu mwenyekiti wa klabu hiyo bwana Ed Woodward wiki hii kwa minajiri ya kufanya majadiliano ya mipango ya usajili mara dirisha la uajili la mwezi January litakapofunguliwa.
 
Louis van Gaal can't watch as his Man United side went down 5-3 at Leicester City on Sunday
 
Van Gaal, anatarajiwa kutumia kiasi cha paundi milioni 64 ili kukiimarisha kikosi chake na kiungo Kevin Strootman likiwa ndio chaguo lake namba moja katika kuimarisha sehemu ya ulinzi wa klabu ya Manchester United.

Mholanzi huyu ameanza kulaumiwa miongoni mwa mashabiki wa klabu ya Manchester United kutokana na mwanzo mbovu wa ligi kufuatia kipigo cha jumla ya magoli 5-3 kutoka klabu ya Leicester City siku ya Jumapili, kipigo ambacho wadadisi wa masuala ya soka wanakifananisha na kipigo cha Daudi na Goliathi ukilinganisha thamani ya vikosi vya timu hizi mbili.

Van Gaal is well stocked up front but he seriously needs to address the issues in defence
 
Japokuwa Van Gaal anatambua kuwa anahitaji kumnunua mlinzi wa kati kuimarisha safu ya Ulinzi ya klabu hiyo lakini bado anamtazama kiungo Mholanzi anayekipiga kwenye klabu ya AS Roma Kevin Strootman, kama ni mmoja wa masuluhisho yake ya kukiimarisha kikosi hicho cha mashetani wekundu.

Post a Comment

 
Top