0
Liverpool 'will offer Sterling more than £100,000-a-week to turn down Real move'
Liverpool imeripotiwa kutaka kumuongeza mshahara mshambuliaji wake Raheem Sterling ili kujaribu kumshawishi asiondoke ndani ya klabu hiyo na kwenda kujiunga na Magalactiko Real Madrid ambao wameonesha nia ya kweli ya kutaka kumsajili mchezaji huyo kwenye dirisah dogo a usajili la mwezi January.

Taarifa zilizozagaa kuwa klabu ya Liverpool haitaki kumpa mshahara mnono mchezaji huyo kwenye mkataba wake mpya atakao saini siku chache zijazo kutokana na hofu ya kumpa mapesa mengi kijana mdogo mwenye miaka 19 zimewafanaya Madrid waingie kazini rasmi kutaka kumsajili mchezaji huyo na kutoa ahadi ya mapesa mengi pasi na kuangalia umri wala athali zinazoweza kupatikana kutokana na malipo atakayoyapata mchezaji mwenyewe.

Lakini wakati Real Madrid wakiitanagaza adhima yao hiyo ya kutaka kumsajili mchezaji huyo ili akaungane na Magalaktiko wengine ndani ya Santiago Bernabeau, Liverpool wenyewe wametangaza kutaka kumpa mshahara mnono wa zaidi ya paundi 100,000 kwa wiki ili kumshawishi mchezaji huyo aendelee kubakia Anfield.

Mkataba wa sasa wa Sterling unaotarajiwa kuisha mnamo mwaka 2017  unamfanya ajinyakulie kiasi cha paundi 30,000 kwa wiki na hivyo endapo Liverpool wataitimiza adhima yao hiyo maana yake mshahara wake utakua umeongezwa mara dufu.

Post a Comment

 
Top