Klabu ya Fenerbahce ya nchini Uturuki imelipotiwa kumuomba mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Liverpool, Dirk Kuyt ajaribu kumshawishi Mholanzi mwenzake Robin van Persie aachane na Manchester
United ili ajiunge na timu hiyo mnamo mwezi wa January.
Kwa mujibu wa gazeti moja la huko nchini Uturuki linedai kuwa Fenerbahce wako katika mipango thabiti ya kukisuka kikosi chao na wana nia ya kutaka kuwajumuisha kikosini wachezaji wanne wenye majina makubwa na Van Persie akiwa mmoja wao.
Klabu hiyo inaonekana kuwa na tumaini kubwa la kumnasa mshambuliaji huyo kutokana na kuwasili kwa mshambuliaji Radamel Falcao kutoka klabu ya AS Monaco kwa mkopo wa muda mrefu hivyo kumuona Van Persie kama ni mmoja kati ya watu wasiotulia ndani ya klabu hiyo.
Raisi wa klabu ya Fenerbahce, Aziz Yildirim, ameliambia gazeti la Hurriyet kuwa timu yao kwa sasa iko vizuri sana lakini kama italazimika basi watawanunua wachezaji watatu au wanne wa kiwango cha juu duniani mwezi January na Van Persie anaonekana kuwa mmoja kati ya wachezaji walengwa.
Hata hivyo Manchester United wanaonekana kutokuwa tayari kutaka kumuuza Van Persie katika siku za usoni licha ya Mashetani wekundu hao kumsainisha Radamel Falcao kutoka klabu ya AS Monaco.
Lakini imethibitika pia meneja wa klabu ya Manchester United, Louis van Gaal hafikirii kumuuza Van
Persie kwani licha ya uwezo wake mkubwa awapo uwanjani lakini pia ni mmoja kati ya wachezaji walio na mahusiano ya karibu sana nao na ikumbukwe ndiye aliyekuwa nahodha wake kwenye kikosi cha The Oranges michuano ya kombe la Dunia kule nchini Brazil.
Post a Comment