0
Daniel Agger ameanika hadharani sababu zilizomfanya yeye aondoka ndani ya klabu ya Liverpool kuwa ni tofauti iliyokuwepo baina yake na meneja wa timu hiyo Brendan Rodgers.

Agger aliondoka ndani ya Anfield na kujiunga na klabu ya Brondby kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 3 mara baada ya kupata nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza cha klabu ya Liverpool kwenye michezo takribani 16 tu kwenye msimu uliokwisha wa Premier League.

Agger amesema mahusiano yake na meneja huyo wa zamani wa klabu ya Swansea Brendan Rodgers yalianza kuwa mabaya mara baada ya kile anachokiita kuwa ni kitendo cha meneja huyo kutokutambua na kuuthamini mchango wake ndani ya klabu hiyo ya Anfield.

“Ngoja nikuambie kitu, mimi na meneja wangu hatukua na mahusiano mazuri hata kidogo katika kipindi chote cha msimu uliopita".

“Mahusiano yetu yalikua ya mbali sana na kwaupande wangu hilo lilinichosha na kunikatisha tamaa kabisa. Sidhani kama alikua akiuthamini na kuutambua mchango wangu ndani ya kikosi chake na hivyo nikaona suluhisho pekee ni kwangu kutafuta muelekeo ambao utanifanya nifurahie kazi yangu". 


Post a Comment

 
Top