Wakati akiwa akisherehekea kutimiza miaka 10 ndani ya klabu ya Manchester United nahodha wa klabu ya Manchester United, Wayne Rooney amesherehekea miaka kumi hiyo kwa kupewa kadi nyekundu mara baada ya kumchezea rafu ya makusudi Stewart Downing.
Kadi hiyo sasa itamfanya Rooney kukaa nje ya uwanja mpaka November 2 hivo kumaanisha kuwa atakwenda kuikosa michezo dhidi ya: Everton (Nyumbani), Westbromich Albion (Ugenini), na mchezo dhidi ya vinara wa ligi ya Uingereza Chelsea (Nyumbani).
Post a Comment