0
Chelsea fan dies after watching Lampard's City equaliser
Frank Lampard (kushoto) aligoma kushangilia goli hilo alilolifunga dhidi ya timu yake ya zamani ya Chelsea 

Mchezaji na mshabiki wa mpira wa miguu mmoja wa nchini Uganda ambaye ni shabiki wa klabu ya Chelsea ametajwa kufariki Dunia kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kushindwa kwa moyo wake kufanya kazi kutokana na kupata mshituko mara baada ya kiungo wa zamni wa klabu ya Chelsea anayekipiga kwenye klabu ya Manchester City kwa mkopo Frank Lampard kuisawazishia Manchester City dhidi ya timu yake ya zamani ya Chelsea.

Fahad Musana aliyekua akiichezea timu ya jeshi ya Simba FC ameripotiwa kuwa alikua akiiangalia mchezo wa Premier League katika eneo la Bombo wakati alipopoteza fahamu na hatimaye kupoteza uhai mara baada ya goli hilo la Lampard la kusawazisha.

Mchezaji mwenzake aliyefahamika kwa jina la Gerald Bagoole, alisema: ‘Tulifanya nae mazoezi siku ya Jumamosi asubuhi, tulikula chakula cha mchana pamoja na hakuonesha dalili yoyote ile ya kuumwa wala kujisikia vibaya".

‘Muda wa mchezo ulipowadia tulikwenda kuutazama mchezo huo karibu kabisa na nyumbani kwake. Alikua ni shabiki mkubwa sana wa Chelsea ambaye alikua tayari kufanya jambo lolote lile kwaajili ya Chelsea, na ukiachilia mbali kamali ambayo alikua akijihusisha nayo mara kwa mara haswa timu yake ilipokua ikicheza".

Kifo cha Musana kimeifanya klabu yake ya Simba kuupeleka mbele mchezo wake dhidi ya Soana hadi mwezi wa October.

Chelsea fan dies after watching Lampard's City equaliser  Andre Schurrle aliifungia Chelsea goli la kuongoza dhidi ya Manchester City katika dimba la Etihad.

Chama cha soka nchini Uganda nacho hakikusita kuanika hisia zake hadharani na kutuma salamu za rambirambi kutokana na kifo cha mchezaji huyo. 

‘Fufa imeshitushwa sana mara ilipopokea taarifa za kusikitisha za kifo cha mchezaji wa klabu ya Simba FC, Musana Fahad kilichotokea Bombo jioni hii,’ taarifa ilisema.

‘Mwili wa mchezaji huyo ulihifadhiwa katika hospitali ya kijeshi ya Bombo kwaajili ya mipango ya mazisi.

Post a Comment

 
Top