Mabingwa wa Serie A, Juventus wanasemekana kuwa kwenye mipango mizito na kabambe ya kutaka kumnyakua kiungo wa klabu ya Manchester United Juan Mata kwenye dirisha dogo la usajili la mwezi Januari.
Muhispania huyo aliyetua Old Trafford miezi tisa iliyopita kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 37 akitokea klabu ya Chelsea, amekua akijaribu kurejea katika kiwango chake cha kawaida ambacho kilimfanya kuwa mchezaji bora wa mwaka wa klabu ya Chelsea kwa miaka miwili mfululizo 2012 na 2013.
Bosi mpaya wa klabu ya Manchester United Mholanzi Louis van Gaal amemjumuisha kikosini mwake mshambuliaji Angel Di Maria kutoka klabu ya Real Madrid kwa ada ya uhamisho iliyovunja rekodi ya uhamisho wa Uingereza kwenye majira haya ya kiangazi jambo ambalo wadadisi wa mambo wanaona linamaanisha kuwa kiungo Juan Mata anaoneshwa mlango wa kutokea ndani ya Manchester United.
Juventus inasemekana wameonesha nia ya kutaka kumsajili mshambuliaji huyo wa zamani wa klabu ya Valencia na wakiamini kuwa thamani yake haitakua juu sana kutokana na klabu yake ya Manchester United kutokuwemo kwenye orodha ya vilabu vinavyoshiriki kwenye mishuano ya vilabu bingwa barani Ulaya yaani UEFA Champions League.
Uhamisho huu unaonekana utawarahisishia klabu ya Manchesta United uwezekano wa kumsajili kiungo raia wa Chile anayekipiga katika timu ya Juventus Artulo Vidal ambaye United imeonesha dhamira ya wazi ya kutaka kumsajili kiungo huyo licha ya kuwa na rekodi mbaya ya kuandamwa na majeruhi ya mara kwa mara.
Post a Comment