Wachezaji wa klabu ya Manchester
United wanalazimika kukabidhi simu zao usiku mmoja kabla ya mechi yoyote watakayokua wanakwenda kucheza ikiwa hiyo ndio sheria mpya ya meneja mpya wa timu hiyo Mholanzi Louis van Gaal.
Sheria hiyo mpya imewekwa na Mholanzi huyo mara tu baada ya kuanza kuyatumikia madaraka yake mapya aliyoyatwaa kutoka kwa David Moyes.
Van Gaal hajaishia hapo kwani pia
amewatahadharisha wachezaji wake kwa kuwaambia kuwa hatamjumuisha
kikosini mchezaji yoyote yule atakayethubutu kuchelewa kwenye kifungua
kinywa (Chai) ya asubuhi ya siku ya mchezo.
Lakini sheria hizi mpya za meneja huyu zinaonekana kutokuzaa matunda
kwani United bado inaendelea kuweweseka na jinamizi la matokeo mabovu
kwani mpaka sasa katika michezo mitatu ya ligi iliyokwisha cheza hakuna
hata mmoja ambao United wamepata matokea ya ushindi.
United wamefungwa kwenye mchezo wa ufunguzi wa ligi dhidi ya Swansea, lakini pia wametoka sare na Sunderland na Burnley bila ya kusahau kipigo cha mbwa mwizi walichokipata kutoka kwa MK Dons cha jumla ya magoli 4:0 kwenye michuano ya Capital One.
Van
Gaal amekua hana taarifa zinazovutia sana kwenye masuala ya kiutawala
kwani ziko taarifa zinazodai kuwa wakati yuko kwenye klabu ya Ajax wachezaji
walikua wakilipishwa faini pindi walipokua wakichelewa kwaajili ya chai
ya asubuhi na walilipishwa mara mbili zaidi walipochelewa kwa mara
nyingine tena.
Post a Comment