Liverpool na Manchester United wamewashiwa taa ya kijani katika mpango wao wa kutaka kumsajili kiungo wa klabu ya Borussia Dortmund Marco Reus, mara baada ya kuthibitika kuwa mazungumzo ya mkataba baina ya timu hiyo na mchezaji yanakwenda polepole mno kuliko vile ilivyokuwa ikidhaniwa hapo awali.
Vilabu kadhaa barani Ulaya vimekua vikimtolea macho Reus katika dirisha lililopita la majira ya joto lakini mchezaji huyo aliamua kubakia kwenye klabu ya Dortmund.
Kwa mujibu wa gazeti la the Express la nchini Uingereza limeandika kuwa,
kipengele cha kuvunja mkataba wa Reus kuanzia mwakani ni paundi milioni 20 jambo ambalo linaacha milango wazi kwa vilabu vilivyokua vikimtazama kwa jicho la tatu mchezaji huyo Liverpool na Manchester United vikiwa vimoja wapo katika mbio hizo.
Arsenal ni moja kati ya vilabu ambavyo vimekua vilifuatilia kwa ukaribu sana mwenendo wa mazungumzo ya mkataba baina ya mchezaji huyo na klabu yake na taarifa za Reus kugoma kusaini mkataba mpya mapaka atakapojua mustakabali wake na wa klabu kwa ujumla huku suala la usajili wa wachezaji na maslahi binafsi likiwa ndio vitu anavyovipa kipaumbele mchezaji huyo vinatoa mwanga mpya wa uwezekano wa kumnasa kiungo huyo.
Robert Lewandowski na Mario Gotze wote wameondoka ndani ya klabu hiyo msimu huu na wamehamia kwa wapinzani wao wakubwa klabu ya Bayern Munich hivyo Reus anataka auone ushawishi kutoka kwa meneja wake Jurgen Klopp ili kuifanya timu hiyo kuwa ya ushindani.
Post a Comment