Mkongwe wa klabu ya Manchester
United David Beckham anaamini kuwa ni huzuni kubwa kumuona Danny Welbeck akiondoka ndani ya klabu ya Manchester United na anaamini kuwa usajili huo ni moja kati ya usajili makini uliofanyika kwenye dirisha hili la usajili la majira ya joto kwa kumjumuisha mshambuliaji huyo kikosini.
Welbeck, mwemye umri wa miaka 23, amekamilisha uhamisho wa paundi milioni 16 siku ya mwisho ya usajili kutoka Manchester United kwenda Arsenal mara baada ya bosi wa Manchester United Louis van Gaal kumwambia mchezaji huyo kuwa anaweza kuenda atakako.
Beckham aliyeichezea England jumla ya michezo 115 na 58 kati ya hizo akiwa nahodha ameifungia Manchester jumla ya magoli
85 katika michezo 394 amesema hajisikii vizuri na anasikitika kumuona mshambuliaji huyo wa
Three Lions (Timu ya taifa ya Uingereza) akienda kumalizia karia yake ya soka nje ya Manchester United.
Post a Comment