Polisi wa jiji la London wamesema wamejipanga kisawasawa kuwakabiri masabiki zaidi ya 5000 wa vilabu vya Galatasaray na Besiktas zote kutoka Uturuki wanaotarajia kutua jijini humo kwenda kuvipa sapoti vilabu vyao kuelekea michezo ya Uefa Champions League na Europa League watakapo vaana na vilabu vinavyotoka jiji la Londoni vya Arsenal na Tottenham wiki hii.
Vilabu hivi ni moja kati ya vilabu vinavyotajwa kuwa na mashabiki wenye vurugu sana na kama unaweza kukumbuka ni kuwa kwenye msimu wa mwaka jana kwenye mchezo wa derby uliokuwa ukivihusisha vilabu kutoka jiji la Istanbul ulivunjika pale ambapo mamia ya mashabiki walipoamua kurusha mawe uwanjani wakati timu ya Galatasaray ikiwa inaongoza kwa jumla ya magoli 2-1 magoli yote yakifungwa na
Didier Drogba.
Polisi walitumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya na kuwaondoa wahuni hao uwanjani na kuwaamuru
Drogba na wachezaji wenzake kuondoka uwanjani hapo mara moja.
Gala
wanakwenda kuwavaa Arsenal kwenye mchezo wa Uefa Champions League kwenye dimba la Emirates siku ya Jumatano, wakati Besiktas wenyewe watavaana na Tottenham kwenye michuano ya Europa League kwenye dimba la White
Hartlane siku ya Alhamisi usiku.
Galatasaray tayari wameshauza jumla ya tiketi 3,000 na takribani tiketi 2,800 zinatarajiwa kuuzwa na klabu ya Besiktas.
Msemaji wa Polisi wa jiji la London amesema: ‘Tunaifahamu historia ya vilabu vyote viwili na hivyo tayari mipango madhubuti tumekwishaiweka kukabiliana na changamoto zote zinazoweza kuletwa na mashabiki hawa. Lakini pia tunatambua kuwa vilabu hivi vina mashabiki wakazi wa Jiji la London."
‘Kama mtu yeyote atakua amejikuta yuko kwenye mazingira magumu au ana jambo lolote lile analotaka kulitolea taarifa, namba yetu mpya ya kutuma ujumbe mfupi wa maandishi ni 61016 ambayo inapatikana muda wote kuanzia sasa.’
Post a Comment