0
San Siro to host 2016 Champions League final
Uwanja wa  Giuseppe Meazza (San Siro) umeteuliwa kuwa ndio uwanja utakao tumika kwaajili ya mchezo wa fainali za UEFA za mwaka 2016 wakati uwanja wa Basel ndio utakaotumika kwa ajili ya mchezo wa fainali ya Europa League.

Giuseppe Meazza, uwanja unaotumika kwa pamoja na vilabu vya AC Milan na Inter Milan, kwa mara ya mwisho ulitumika kama mwenyeji wa fainali hiyo mnamo msimu wa UEFA wa mwaka 2000-01, wakati Bayern Munich walipokipiga dhidi ya Valencia.

Uefa pia imekitaja kiwanja cha klabu ya FC Basel cha  St Jakob Park kuwa ndio kitakachotumika kama kiwanja mwenyeji kwaajili ya mchezo wa fainali ya Uefa Europa League katika msimu huo wa mwaka 2015-16.

Post a Comment

 
Top