0
Done deal: Manchester United have won the race to sign Radamel Falcao from Monaco on a loan deal
Manchester United wameshinda mbio za kumsainisha mshambuliaji wa klabu ya AS Monaco ya huko nchini Ufaransa Radamel Falcao kwa mkataba wa mkopo wa mwaka mmoja.

Mshambuliaji huyu ataighalimu klabu ya Manchester United kiasi cha paundi milioni 12 na sasa anakwenda kuungana na Angel di Maria, Daley Blind, Luke Shaw, Ander Herrera na Marcos Rojo katika kikosi cha Mholanzi Louis van Gaal wa Manchester United.

 Sitting it out: Falcao (right) watched Monaco's game against Lille from the stands at the weekend

Kinachosubiriwa kwa sasa ni makubaliano binafsi baina ya Falcao na Manchester United kwani tayari United na Monaco wamekwisha fanya makubaliano yote ya kimsingi kuhusiana na uhamisho wa mchezaji huyo.

Taarifa zinasema kuwa klabu ya Manchester United iko tayari kumpatia mshahara mnono wa kiasi cha paundi 200,000 kwa wiki na tayari taarifa zisizo rasmi zinadai kuwa mchezaji huyo yuko kwenye ndege binafsi kutoka nchini Ufaransa kuelekea jijini Manchester kukamilisha uhamisho wake.



Post a Comment

 
Top