Mshambuliaji Mjerumani anayekipiga kwenye klabu ya Arsenal Lukas Podolski ameonesha wasiwasi wake wa kukosa sapoti kutoka kwa meneja wa klabu yake Mfaransa Arsene Wenger.
Podolski amethibitisha kuwa yuko katika wakati mgumu sana ndani ya klabu hiyo mara baada ya timu hiyo kumsajili Dany Welbeck siku ya mwisho ya kufungwa kwa dirisha la usajili akitokea klabu ya Manchester United na amesema kuwa hana uhakika kama atapata nafasi ya kukitumikia kikosi cha Mfaransa huyo.
Podolski ametanabahisha kuwa inakuwa ni vigumu sana kwa timu kumnunua mchezaji kwa mapesa lukuki na mwishowe kumuweka nje ya uwanja basi na sababu yoyote ile na hivyo anajiona kuwa yuko katika wakati mgumu sana kutokana na ujio wa mshambuliaji huyo wa Kiingereza.
Lakini Poldolski ameendelea kujipa imani kwa kusema kuwa bado wana msimu
mrefu sana mbele yao na kusema kuwa muda ndio utakao zungumza kuhusiana
na nani anastahili kukabidhiwa jukumu la kuiongoza klabu hiyo katika sehemu ya ushambuliaji.
"Ninapokuwa vizuri bila ya maumivu huwa najiona kuwa mimi ni mtu sahihi sana ndani ya kikosi cha Arsenal na najiona kama sina mpinzani katika kikosi cha watu 11 wa mwanzo wa timu yangu japo wakati fulani mambo huwa tofauti sana.
Alipoulizwa kama anadhani anaaminiwa na meneja wake Podolski alisema hana uhakika na hilo na anadhani muda na uwezo ndio utazungumza nani wa kuaminiwa na nani wa kutumika ndani ya Arsenal.
Post a Comment