Dirisha la usajili la majira haya ya kiangazi kwa vilabu majira haya ya kiangazi limefungwa hapo jana usiku tukishuhudia miezi kadhaa ya kufuru ya matumizi yaliyokithili ya pesa kwa vilabu barani Ulaya.
Japokuwa rekodi ya uhamisho ghali zaidi duniani inashikiriwa na Gareth Bale ya uhamisho wa Euro milioni 100 alipohama kutoka Tottenham kwenda Real Madrid mwaka uliopita lakini mado suala la matumizi ya fedha na uvunjwaji wa rekodi mbalimbali linabakia palepale kwa vilabu kadhaa barani Ulaya.
Wakati vilabu vikiendelea kusharehekea mapato makubwa kwenye matangazo na mauzo ya vifaa mbalimbali isivyo kawaida na vikienda kwenye duka kuu la ununuzi wa wachezaji ambalo ni michuano ya kombe la Dunia iliyofanyika kule nchini Brazil, Vilabu vinaonekana kuongeza ushindani pia kwenye matumizi ya mapato hayo makubwa wanayojikusanyia kupitia vyanzo mbalimbali vya mapato.
Ufuatao ni usajili wa wachezaji kumi ambao wamenunuliwa kwa mahela mengi kwenye msimu huu wa manunuzi.
TOP 10 MOST EXPENSIVE TRANSFERS OF SUMMER 2014
No. | Mchezaji | Kutoka | Kwenda | Ada (Euro) |
1 | Luis Suarez | Liverpool | Barcelona | 88m |
2 | James Rodriguez | Monaco | Real Madrid | 80m |
3 | Angel Di Maria | Real Madrid | Manchester United | 75m |
4 | David Luiz | Chelsea | Paris Saint-Germain | 49.5m |
5 | Eliaquim Mangala | Porto | Manchester City | 44.5m |
6 | Diego Costa | Atletico Madrid | Chelsea | 44m |
7 | Alexis Sanchez | Barcelona | Arsenal | 40m |
8 | Luke Shaw | Southampton | Manchester United | 37.8m |
9 | Ander Herrera | Athletic Bilbao | Manchester United | 36.5m |
10 | Cesc Fabregas | Barcelona | Chelsea | 36m |
Post a Comment