0
Raisiwa shirikisho la soka barani Ulaya (UEFA) Michel Platini amesema Franck Ribery anaweza kuadhibiwa na shirikisho hilo endapo tu itathibitika kuwa aliitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa na akaukataa wito huo wa mwalimu Didier Deschamps.

Ribery alitangaza kuachana na soka la kimataifa mara baada ya kulitumikia taifa hilojumla ya michezo 81 na aliikosa michuano ya kombe la Dunia ya mwaka huu kule nchini Brazil kutokana na maumivu ya mgongo.

Ufaransa imepoteza matumaini ya kumtumia mchezaji huyo wa mabingwa wa ligi ya Ujerumani Bayern Munich licha ya mwalimu a timu hiyo ya Ufaransa kutamka hadharani kuwa milango bado ikowazi kwa Ribery kulitumikia taifa lake haswa katika kampeni hizi za kuwania nafasi ya kucheza michuao ya Ulaya ya mwaka 2016 ambapo Ufaransa ndiye anatarajiwa kuwa mwenyeji.

Ribery sasa anweza kukumbana na adhabu ya kufungiwa kuitumikia timu yake ya Bayern endapo tu itathibitika kuwa ni kweli alikaidi kuitikia wito wa mwalimu Deschamps wa kujiunga na kikosi cha timu ya taifa ya Ufarasa amethibitisha raisi huyo wa UEFA ambaye pia ni mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa.

"Sifahamu lolote kuhusiana na hili," Platini aliliambia gazeti la Ujerumani Bild. "Si maamuzi ya mchezaji, kama atajiunga na timu au kutokujiunga. Ni maamuzi ya kocha wa timu na ndio mwenye mamlaka ya mwisho katika hilo".

"Ribery hawezi kujiamlia kama anaweza kujiunga na timu au kutokujiunga nayo. Kama mwalimu Didier Deschamps alimjumuisha kikosini ni lazima ajiunge na timu bila ya kukosa.

"Hili limo kwenye sheria za UEFA na FIFA pia. Limeelezewa kwa mapana na marefu kuwa endapo itathibitika kuwa hakujiunga kwa makusudi basi atatakiwa kuitumikia adhabu ya kukosa michezo mitatu kwenye klabu yake ya Bayern Munich".


Post a Comment

 
Top