0
Zidane faces six-month ban if found guilty of coaching without correct licence
Zinedine Zidane akatakiwa kutumikia kifungo cha miezi cha kutojihusisha na masuala ya mpira wa miguu endapo tu itathibitika kuwa anafanya kazi yake ya ukocha wa kukinoa kikosi B cha Real Madrid bila ya kuwa na leseni halali. 

Chama cha makocha nchini Uhispania (CENAFE) kimeonekana kulitilia shaka jambo hili kuhusiana na vyeti vya kufundishia vya nguli huyo wa zamani wa Ufaransa na Los Blancos.

Taarifa zinasema kuwa Zidane amekuwa akitumika kama kocha mkuu wa timu B ya Real Madrid licha ya ukweli kwamba bado Zizou hajapeleka vyeti vyake kwenye bodi hiyo ya makocha.

Nyaraka na picha za video zimetumwa kwenye kamati ya mashindano ya chama cha soka cha nchini Hispania zikimuonesha Zizou akitoa mafunzo kwa kikosi B cha Real Madrid ili zitumike kama ushahidi wa kumtia hatiani Zidane licha ya klabu ya Real Madrid kudai kuwa Zidane anamsaidia kocha mkuu wa kikosi B Sergio Sanchez.

Kamati sasa iko inapitia nyaraka hizo za Zidane na Real ili kujiridhisha kama wamevunja sheria namaba 104, ambayo hukumu yake ni kufungiwa kati ya michezo minne (4)  hadi ishirini (20) au mwezi mmoja (1) hadi sita (6).

Post a Comment

 
Top