Kiungo wa klabu ya Borussia
Dortmund, Nuri Sahin anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa kipindi kisichopungua miezi miwili kutokana na kufanyiwa upasuaji wa kifundo cha mguu hii leo.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 25 raia wa Uturuki aliyerejea kwenye klabu ya Dortmund mnamo mwaka 2013
mara baada ya kuwa na misimu mibovu akiwa na vilabu vya Liverpool na Real Madrid, alikokuwa anavitumikia kwa mkopo amefanyiwa upasuaji huo ambao inasemekana umefanyika kwa usalama.
Katika taarifa hiyo iliyotolewa na dakatari wa klabu ya Borussia Dortmund Markus Braun amesema kuwa mchezaji huyo anatarajiwa kuwa nje kwa kipindi kisichopungua miezi miwili.
Dortmund,
ambao wamemaliza katika nafasi ya pili ya ligi kuu ya nchini Ujeruman almaarufu kama Bundesliga kwenye msimu uliokwisha pia ni miongoni mwa timu zinazoshiriki michuano ya vilabu bingwa barani ulaya na kwa msimu huu imepangwa kwenye kundi D pamoja na vilabu vya Arsenal ya Uingereza, Galatasaray ya Uturuki na Anderlecht ya Uberigiji.
Sahin sasa anaungana na wachezaji wengine wa Dortmund kama Ilkay
Guendogan, ambaye hajaitumikia klabu hiyo tangu mwaka uliopita, Jakub Blaszczykowski na Marcel Schmelzer katika orodha ya majeruhi wa klabu hiyo.
Post a Comment