Cristiano Ronaldo amesema angependa kurejea tena ndani ya kikosi cha Manchester United kabla ya kutundika daruga zake muda utakapokua umewadia, lakini akianika hadharani kwa kusisitiza kuwa hafikirii kuondoka ndani ya Real Madrid siku za hivi karibuni.
Ronaldo's aliyewahi kuwa na wakati mzuri ndani ya kikosi cha Mashetani wekundu hao alimaliza wakati wake huo kwenye msimu wa majira ya kiangazi ya mwaka 2009 pale alipohama kwa uhamisho ambao ulivunja rekodi ya dunia kwa kitita cha paundi milioni 80 alipojiunga na Los Blancos.
Ronaldo amenukuliwa na gaazeti la Daily Mail la huko nchini Uingereza akitanabahisha kuwa anaipenda klabu ya Manchester na hilo amekwisha lisema mara kadhaa na kila mmoja anatambua hilo kuwa yeye ni shabiki namba moja wa klabu hiyo.
"Manchester iko moyoni mwangu, nimeacha marafiki zangu wengi sana pale, mashabiki ni waajabu na wenye mapenzi makubwa kwa wachezaji wao na ninatumaini nitarejea pale siku moja kabla sijaamua kutundika daruga zangu".
"Nina furaha ndani ya Real Madrid na nina miaka minne zaidi ya kuwepo hapa kutokana na mkataba wangu mpya niliosaini siku za hivi karibuni, lakini kwa wakati ujao huwezi jua kwani kwa sasa ninatendewa mema sana ndani ya Real lakini kiukweli ninapendelea zaidi kuwepo Manchester United".
Ronaldo pia hakusita kuzungumzia hali ya mambo ilivyokuwa ndani ya klabu ya Manchester United mara baada ya kujiuzuru ghafla kwa aliyekuwa Meneja wa timu hiyo Sir Alex Ferguson iliyejiuzuru mnamo mwezi May 2013.
Angel di Maria na Radamel Falcao ni miongoni mwa wanandinga wakubwa waliotua ndani ya kikosi cha United kwenye majira haya ya kiangazi na Ronaldo kwa mapana na marefu hakusita kuuzungumzia ujio wa wanandinga hao ndani ya klabu yake hiyo ya zamani.
"Amini nakuambia kuwa Manchester United itakua vizuri msimu huu, ninauhakika na hilo, ni klabu kubwa. Wakati mbaya na mzuri ni vipindi vinavyotokea ndani ya klabu kwa nyakati tofauti. Msimu uliokwisha haukuwa mzuri sana kwao na hata msimu huu hawajaanza vizuri sana lakini amini watakaa vizuri na kurejea katika makali yao msumu huu".
"Kwa mtazamo wangu naona wamefanya jambo la maana sana kuwanunua Di Maria na Falcao. Wataimarisha timu natamani kuwaona wakiwa imara kwani wako ndani ya klabu kubwa inayohitaji watu wakubwa na imara pia. Falcao ni mchezaji mzuri sana na ni usajili mzuri sana kwa United, Sitaki kumzungumzia Di Maria kwani huyo ninamfahamu sana ni mtu wa aina gani anapokuwepo ndani ya klabu"
Post a Comment