Kiungo wa klabu ya Arsenal Mesut Ozil anasakwa kwa udi na uvumba na klabu ya Bayern
Munich kuelekea kwenye dirisha la usajili la mwezi January.
Kwa mujibu wa gazeti la The Evening Standard limeandika kuwa mabingwa hao wa Ujerumani wamekua wakimfuatilia kwa ukaribu sana kiungo huyo wa klabu ya Arsenal aliyesajiliwa kutokea klabu ya Real Madrid mnamo mwaka 2013.
Inadaiwa kuwa kocha wa Bayern Pep Guardiola anaamini kuwa atafanikiwa kumpata kiungo huyo kutoka klabu ya Arsenal endapo tu atatuma ofa kubwa kwa klabu hiyo mnamo mwezi January huku suala la mchezaji mwenyewe kuonekana hana utulivu ndani ya klabu hiyo likimpa matumaini zaidi.
Inasemekana kuwa kitendo cha mchezaji huyo kuchezeshwa nafasi tofauti na kiungo mshambuliaji inamfanya awe katika wakati mgumu sana na hivyo kuongeza chumvi kwenye kidonda.
Post a Comment