Arsenal wamerejea katika mstari mwaka huu wakiwa na kikosi chenye marekebisho na sura mpya kadhaa wa kadha. Baadhi ya wachezaji wanaonekana kuchukua mishahara mikubwa sana lakini kwa sasa wanaonekana kama hawana mchango wa kutosha ndani ya klabu.
Kwa mtazamo wangu naona wachezaji wafuatao wangeondoka ndani ya klabu hiyo kwani ukiwatazama wachezaji hao wanakaribia umri wa miaka 30 kwa sasa lakini pia kwa siku za hivi karibuni uwezo wao wa kusakata kabumbu umeshuka sana.
1) Lukas Podolski.
Podolski hajapata kabisa muda wa kucheza msimu huu, lakini pia labda mimi na wewe tuulizane ni lini Mjerumani huyu amewahi kucheza kwa kiwango cha juu sana ndani ya klbu ya Arsenal.
Akiwa na umri wa miaka 29 Podolski ni miongoni mwa wachezaji wanaolipwa zaidi kitu ambacho naona kwa upande wa klabu ya Arsenal sidhani kama wataweza kukiendeleza.
Msahahara wa Podolski ni paundi elfu 95 kwa wiki na nadhani dirisha la usajili la mwezi January litakua wakati mujarabu sana kwa mchezaji huyu kuondoka na Arsenal wanaweza kupigana kuinasa saini ya Marco Reus kama mbadala wake katika kuziba pengo hilo litakaloachwa na Poldoski.
2) Tomas Rosicky.
Mchezaji huyu wa kimataifa wa Jamuhuri ya Czech bado yuko katika kiwango cha juu kiasi lakini nilipomtazama siku ya juzi niligundua kuwa ni mchezaji anayehitaji kuchezeshwa mara kwa mara ili kukilinda kiwango chake.
Kwa sasa nafasi ya Rosicky hawezi kupata nafasi mara kwa mara kutokana na changamoto ziliopo sasa ndani ya klabu ya Arsenal hivyo lililo bora kwake kwa sasa ni kutafuta nyumba nyingine itakayomfaa.
Mshahara wa Tom ni paundi 85,000 kwa wiki, nadhani wakati muafaka kwake kuondoka ni mwishoni mwa msimu huu na nafasi yake haihitaji manunuzi yoyote yale kwani wako vijana chipukizi wengi sana ndani ya klabu ya Arsenal ambao wanaweza kuliziba pengo lake.
3) Mikel Arteta.
Arteta ndiye nahodha wa Arsenal wa sasa na nadhani jambo muhimu kwake kwa sasa ni kuangalia mkataba wake na sidhani kama kuongeza mkataba na Arsenal litakua jambo la busara kwake kwani nionavyo mimi ni kuwa siku zake za kucheza katika kiwango cha juu zinahesabika kutokana na umri kuanza kumtupa mkono kwani unaweza ona hata sasa ameanza kutumika kama kiungo mkabaji nafasi ambayo kiasili si ya kwake.
Mshahara wa Arteta ni paundi 80,000 kwa wiki na nadhani wakati wake muafaka kuondoka ni mwishoni mwa msimu na anayeweza kuwa mbadala wake ni kiungo wa kiwango cha juu yoyote yule duniani mwenye uwezo wa kucheza kwenye klabu kubwa kama Arsenal na William Carvalho au Lars
Bender ni watu ambao wanaweza wakawa mbadara muafaka wa Arteta.
4) Mathieu Flamini.
Flamini ni mchezaji muhimu sana lakini hali yake ya kiafya haimruhusu kutumika mara kwa mara kwani ameshakua akisumbuliwa mara kwa mara.
The Gunners wanahitajio kubwa sana kutoka kwa Flamini lakini hajaonesha dalili za kutaka kuwapa raha mashabiki wa Arsenal kutokana na uwezo wake anaouonesha kwa sasa.
Mshahara wa Flamini ni paundi 65,000 kwa wiki na nadhani mwezi january ni wakati muafaka sana kwake kutimuka ndani ya kikosi hicho na Adrien Rabiot anaweza kuwa mtu muafaka kuziba pengo lake lakini endapo Diaby atakua fiti kwa asilimia mia basi nadhani tatizo litakua limetatuliwa.
Post a Comment