Meneja wa timu ya Borussia Dortmund Jurgen
Klopp amekanusha taarifa zilizotolewa kwamba mchezaji wake Ilkay Gundogan
aliyekua akisumbuliwa na majeruhi ya muda mrefu anatarajiwa kurejea siku ambayo timu yake ya Borussia Dortmund itakapomenyana dhidi ya Vfb Stuttgart.
Kiungo huyo anayesumbuliwa na maumivu ya mgongo ameendelea kujiuguza na maumivu hayo yanayomsibu na juzi kuliibuka taarifa kuwa mchezaji huyu yuko tayari sasa kurejea uwanjani siku timu hiyo itakapokipiga dhidi ya Stuttgart katika dimba la Signal-Iduna Park.
"Siku ambayo Ilkay Gundogan atarejea mchezoni litakua jambo kubwa kwa kila mmoja wetu ," Alisena Klopp.
Post a Comment