0
Jana aliyewahi kuwa meneja wa klabu ya Manchester united Sir Alex Ferguson alikuwa akifanya mahojiano na moja kati ya vituo vya televisheni nchini Uswisi wakimuhoji kuhusiana na muelekeo wa tasnia ya soka barani Ulaya na Duniani kwa ujumla na moja kati ya maswali aliyoulizwa ni kuhusiana na matumizi makubwa ya pesa yaliyooneshwa na klabu yake ya Manchester United aliyokua akiiongoza tofauti na ilivyokua enzi za utawala wake.

Moja kati ya mambo yaliyojitokeza ni kuibuka kwa wakala Jorge Mendes kuwa ndiye anayefanikisha madili makubwa ya uhamisho wa wachezaji wakubwa na chipukizi Duniani na bila ya kusita kibabu hakikusita kuweka wazi kuwa huyu ni mmoja kati ya mawakala wenye sifa na wasio wababaishaji ambao yeye amekwishawahi kufanya kazi nao katika karia yake ya masuala ya mpira awa miguu.


Discussions: Mendes chats with Monaco's sporting director Vadim Vasilyev at a Ligue 1 game this season

Furguson alimsifu wakala huyu kuwa ni wakala asiyekuwa mbabaisaji lakini anayehakikisha kuwa anafuatilia maendeleo ya wachezaji wake wakati wote.

Amekua akiingilia kati kila pale amabapo amekua akigundua kuwa mteja wakae amekua hatendewi kulingana na makubaliano ya awali ya mkataba wake na klabu hiyo tofauti na ilivyo hapakwetu ambapo mawakala wametokea kuwa ni moja kati ya wababaishaji wakubwa.

Imefikia wakati kwa hao wanaojiita mawakala wamekua wakiwashawishi hao wateja wao wazitoroke kambi za timu zao ikiwemo ya Taifa alimradi wao awaendelee na kupata maslahi yao ya kimaisha.

Chelsea manager Jose Mourinho looks on as he enters his car after attending a two-day meeting of the UEFA Elite Club Coaches Forum

Mendes ndiye aliyempeleka Cristiano Ronaldo mnamo mwaka 2003 kwenye klabu ya Machester United wakati huo ikiongozwa na Ferguson kabla ya baadae kumletea Luis Nani, Olivieira Anderson na Bebe.

Lakini Mendes ndiye aliyefanikisha dili la kumsainisha Diego Costa kwenda kwenye klabu ya Chelsea bila ya kusahau idadi ya wachezaji lukuki ambao alimsaidia kocha Mourinho kuwanasa akiwa katika vilabu vya Chelsea, Inter Milan na  Real Madrid kwa nyakati tofauti


Lakini kupitia wakala huyu klabu ya Atletico Madrid ilifanikiwa kujipatia kitita cha paundi milioni 48 kutoka kwa klabu ya AS Monaco ya nchini Ufaransa kwaajili ya saini ya mshambuliaji Radamel Falcao kwenye majira ya kiangazi ya mwaka 2013.

 Radamel Falcao of Atletico Madrid celebrates scoring his team's second goal during the UEFA Europa League Final between Atletico Madrid and Athletic Bilbao at the National Arena in Bucharest, Romania.

Sahau kuhusu  Falcao, Mendes ndiye aliyefanikisha uhamisho wa James Rodriguez kutoka klabu ya FC  Porto kwenda klabu ya  Monaco kwa ada ya paundi milioni 40 kabla ya yeye mwenyewe tena mwaka mmoja zaidi kusimamia dili la uhamisho wa paundi milioni 63 la James Rodriguez kujiunga na magalaktiko wa Real Madrid.

Halikadhalika dili la Meneja Jose Mourinho kujiunga na klabu ya Real Madrid kwa kiasi kikubwa lilihusisha nguvu zake yeye kabla ya kutumia ushawishi wake wa kuwanansa wachezaji Simon  Pepe, James Rodriguez, Fabio Coentrao na Christiano Ronaldo kujiunga na Les Blancos.


Ronaldo, kwa sasa ana mkataba wa miaka minne na Real na ametamka hadharani kuwa anajisikia furaha sana kuwepo ndani ya klabu hiyo lakini kauli yake aliyoitoa siku ya Jumaatano iliyopita kuwa anaamini kuwa iko siku atarejea ndani ya klabu ya Manchester United inazusha hofu miongoni mwa washabiki wa Real kutokana na vile wakala wake Mendes anavyofanya kazi kwa kuangalia upepo wa fedha kwake na kwa mchezaji wake.

Ufanyaji kazi wa wakala huyu hauna mahusiano yoyote na upinzani wa vilabu hata vya mji mmoja kwani ukiachilia mbali mazuri yote aliyowatendea United kiasi cha kusifiwa na Furguson lakini pia msimu huu amefanikisha dili la klabu ya Manchester City kumnasa Eliaquim Mangala, kutoka klabu ya FC Porto, kwa ada ya uhamisho inayotajwa kuwa ni paundi milioni 32.


 Wakala huyu amefanikisha usajili wa masuper star kibao kujiunga na vilabu mbali mbali na msimu huu amefanikisha dili la uhamisho wa masuper star wafuatao

1. James Rodriguez.

 

Mara baada ya kung'ara kwenye michuano ya kombe la Dunia kule nchini Brazil akiwa na kikosi cha Colombia, Rodriguez amekamilisha uhamisho wa ndoto zke kutoka klabu ya Monaco kwenda  Real Madrid kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 63.

2. Angel Di Maria


Baada ya klabu ya Madrid kushindwa kumpa mkataba aliokuwa akiutaka Di Maria, Muargentina huyu aliamua kutua Old Trafford kwa ada inayosemekana kufikia paundi milioni 59.7.

3. Diego Costa.

 On target: Chelsea striker Diego Costa, another Mendes client, has already scored four Premier League goals

Amehama kutoka klabu ya Atletico Madrid mara baada ya kuwa na msimu bora kabisa kwenye La Liga lakini hatimaye mchezaji huyu amejiunga na Chelseakwa ada ya uhamisho wa paundi milioni 35.

4. Eliaquim Mangala.

 On the move: Defender Eliaquim Mangala joined Premier League champions Manchester City this summer


Mlinzi Mfaransa Eliaquim Mangala amenunuliwa akitokea klabu yab FC  Porto kwenda klabu ya Manchester City kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 35.

5. Radamel Falcao.

 All smiles: Mendes poses with Falcao and the Colombian striker's lawyers Paulo Rendeiro and Varlos Osorio

Hii ndio habari ya mjini kwa sasa kutokana na namna uhamisho ulivyokamilika siku ya mwisho ya dirisha la usajili huko nchini Uingereza ambapo Falcao alisaini kuitumikia klabu ya Manchester United kwa mkopo wa muda mrefu wenye thamani ya paundi milioni 6 kutoka klabu ya Monaco.

Tofauti na ilivyo hapa kwetu mawakala wameshindwa kabisa kutupatia matunda ya kazi yao kutokana na ubabishaji uliokithili miongoni mwao kwani mingi ya mikataba wanayoingia na wchezaji hawa imekua ni mikataba ya ulaghai kama ule wa Chifu Mangungo wa Msovero.

Leo hii Watanzania tunakosa jibu linalofanana kuhusiana na dili la Haruna Moshi (Boban), lakini tunakosa jibu la moja kwa moja kwanini mchezaji Thomas Ulimwengu aache kuendelea na majaribio yake aliyokuwa akiyafanya nchini ujerumanai na kuamaua kurudi kabla ya kujiunga na TP Mazembe?

Ziko taarifa zinazodai mawakala wamekua wakinufaika zaidi ya wachezaji wetu hali ambayao waliowengi wameamua kuivunja mikataba yao na hatimaye kubakia wakijiongoza wao wenyewe katika kuingia katika kusaini madili mbalimbali.

Nionavyo mimi ubovu huu unaanzia kwa watawala wenyewe wa soka wa nchi hii yaani TFF, kwani wao ndio wamekua wababaishaji namba moja katika utendajiwa wa  shughuli zao za kila siku za kuendeleza mpira wa miguu katika nchi hii.

Kila kukicha kichwa changu kimekua na maswali mengi yanayokosa majibu kuhusiana na mwenendo wa soka letu kwa ujumla na lini nasi tutakaa nyuma ya luninga zetu tukiwatazama Watanzania wenzetu wakitekeleza majukumu mbalimbali katika vilabu vyao barani Ulaya  kutokana na mambao kadha wa kadha yanayojiri kwenye mpira wetu.

Najaribu kufikiria nguvu kubwa na pesa nyingi zilizotumika katika programu ya maboresho ya Taifa Stars na matunda yaliyopatikana na kugundua kuwa ni moja kati ya mipango isiyo na tija iliyowahi kutokea hapa nchini kwetu na ilikua ni programu ya kujivunia pesa kwa viongozi wa TFF na washirika wao waliowateuwa.

Michuano ambayo mimi naami kama ingeendeeshwa kwa ufasaha ndio ingekua mwarobaini wa soka letu ni michuano ya  Copa Cocacola lakini bahati mbaya iliyoikumba michuano hii ni kuwa imekua haina mfumo ambao ni rasmi kwani imekua ikibadilishwa mfumo wa uendeeshwaji wake kila kukicha kutokana na matakwa ya watawala pasi na kuwahusisha wadau.

Ruvuma anatakiwa acheze dhidi ya Njombe kwenye mechi za mikondo miwili ya nyumbani na ugenini na mshindi anatakiwa aende kwenye fainali ya michuano hii kule jijini Dsm.

Swali linalobakia vichwani mwa wadadisi wa masuala ya soka ni kua je wapi vipaji vitakavyokosa nafasi ya kusonga mbele kuelekeas jijini Dsm vitaelekea mara baada ya michezo hiyo miwili kukamilika ikiwa hawatapata nafasi ikiwa leo hii sina uhakika mahali vilipo vipaji vya akiana Jukumu Kibanda, Godifrey Kumbukila na Nasoro Mhagamma?

Kila kiongozi anayeingia madarakani TFF amekua akiingia na sera zake na nyingi kati ya sera hizo zimekua hazina matunda mbele ya macho ya Watanzania kwani kumekua na mambo mengi ya kibabaishaji katika mihimili ya watawala hawa wa soka la Kinbongo.

Ligi daraja la pili imerejeshwa ghafla tena nadani bila ya vilabu husika kupewa taarifa ya muda mrefu. jambo hili linaniacha mdomo wazi kwani najaribu kuangalia awezekano wa ndugu zangu Wayao wenzangu wakuitunduru wanaoendeesha masualaya soka kwa kutegemea bakuli wanavyoweza kusafiri kwenda Morogoro na Mbeya wakati wanakosa mfadhili anayeweza kuwapatia hata kiasi cha shilingi laki tatu kwa mwaka.

Kwa ubabaishaji huu unaotoka kwa viongozi wakuu sitarajii kuwapata mawakala watakao kuwa na tija katika soka la Bongo ilihali baba mwenyewe anayetakiwa kutazama hakiza wanawe akiwa mbabaishaji pia.

                              HOSSAM HASSAN ULAYA.
                                   hossamulaya@gmail.com
                                     0755231571/0713281932

Post a Comment

 
Top