Wakati Aaron Ramsey na Mikel Arteta wakitarajiwa kuwa nje kwa kipindi cha takribani mwezi mmoja, sehemu ya kiungo ya klabu ya Arsenal inaonekana kukumbwa na majanga makubwa sana kutokana na maumivu ya viungo hao mahiri.
The Gunners tayari wameshaonesha mapungufu makubwa kwenye sehemu ya kiungo cha ukabaji katika kipindi ambacho wachezaji hawa wawili wakiwa hawajakumbwa na majeruhi, lakini maumivu ya Ramsey na Arteta yanaifanya Arsenal kwa kiasi kikibwa kuwategemea Mathieu Flamini na Abou Diaby ambao wanaonekana kutokuwa suluhisho la kutosha.
Flamini anatosha sana kuziba mapengo hayo yaliyoachwa wazi lakini Diaby haonekani kuwa msaada kwa timu yake kutokana na maumivu ya muda mrefu yaliyokuwa yakimkabili hivyo kuhitaji muda zaidi kurejea njiani.
Mathieu Debuchy angeweza kuwa sehemu ya suluhisho lakini nae ni kama vile kisicho lidhiki kwani yeye ameingia kwenye kundi la majeruhi wa muda mrefu ndani ya klabu hiyo.
Klabu ya Arsenal ina jammbo moja tu lakulifanya kwa sasa, nalo ni kumsajiri Lassana Diarra ambaye mimi namuona kama suluhisho kwani ukiachilia mbali uwezo wa kucheza kama kiungo mkabaji pia anaweza kutumika kama mlinzi wa pembeni ndani ya klabu yoyote ile.
Diarra mwenye umri wa miaka 29 yuko katika mchakato wa kutafuta klabu mpya kwa sasa mara baada ya mkataba wake na klabu ya Lokomotv Moscow na alikaribia kujiunga na klabu ya Queens Park Rangers kwenye siku ya mwisho ya usajiri ya majira ya joto yaliyopita.
Arsene Wenger ni shabiki mkubwa wa Diarra na alishawahi kumsajiri mnamo mwaka
2007. Kiungo huyu raia wa Ufaransa hakupata nafasi ya kutosha ya kucheza na hivyo aliamua kuachana na Arsenal mapema sana kabla ya kipaji chake kumalizikia benchini.
Licha ya kutokuwa na wakati mzuri akiwa na The Gunners, Diarra alitimkia klabu ya Real Madrid, ambako alikwenda kuonesha ubora aliokuwa nao hasa katika suala zima la ukabaji.
Wanachoweza kukifanya Arsenal kwa sasa ni kumpa mkataba wa muda mfupi Lass utakaomalizika mwishoni mwa msimu huu ambapo naamini Diarra ataitumia fursa hiyo kuudhihirishia ulimwengu kiasi cha ubora alichonacho kutoka kwa mchezaji huyu ambaye mimi ninaamini kuwa ni mmoja kati ya viungo bora kabisa kuwahi kutokea Duniani kwa sasa katika sehemu ya kiungo cha ukabaji.
Arsenal sidhani kama wanaweza kupambana kwenye nafasi nne za juu kwa kuwategemea Diaby na Flamini kuanzia mwezi ujao mara baada ya kurejea kutoka kwenye majeraha yao, na hata pale ambapo Arteta atakaporejea bado mchezaji huyu kwa sasa anakosa ubora wake wa kawaida ambao mimi na wewe tukiwa kama mashabiki na wafuatiliaji wakubwa wa EPL tunaufahamu.
Licha ya kuwa Diarra anaonekana kuwa ni mfupi kutokana na kuwa na urefu wa futi 5 na nchi 8 bado uwepo wake ndani ya Arsenal utaleta aina fulani ya ushindani na uimara katika sehemu ya kiungo ya klabu ya Arsenal.
Post a Comment