Taarifa zinasema kuwa meneja wa timu hiyo Muingereza Brendan Rodgers amekua akimfuatilia kwa makini mshambuliaji huyo ambaye anaonekana kuto kuwa na utulivu ndani ya klabu hiyo.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Argentina alijiunga na Napoli mwaka mmoja uliopita akitokea klabu ya Real Madrid anaonekana kuto kujiamini sana na maisha yake ndani ya klabu ya Napoli kutokana na taarifa zilizo zagaa kuwa mwalimu wa zamni wa klabu ya Manchester City Roberto Mancini anatarajiwa kwenda kuchukua nafasi ya mwalimu wa sasa wa Napoli Rafa Benitez.
Post a Comment