Siku chache tu mara baada ya kurejea nchini Engaland kwenye EPL mchezaji mwenye vituko na matukio mengi ya ajabu nje na ndani ya uwanja Mario Balotelli amevitikisa tena vyombo vya habari kwa kumunua mjengo wenye thamani kubwa na wenye vikolombwezo vingi kikiwemo kiwanja cha mpira wa miguu.
sehemu maalum ya kutulie helcopta (helipad)
Mshambuliaji huyu mpya wa klabu ya Liverpool aliyesajiliwa kwa ada ya uhamisho wa paundi milioni 16 akitokea klabu ya AC Milan alikua kwenye mawindo mazito ya kutafuta hifadhi tangu aliporejea nchini Uingereza na mwishowe akachagua nyumba moja iliyo kaskazini mwa jiji la Liverpool iliyomghalimu kiasi cha paundi milioni 4.7 kuwa ndio makazi yake ya kudumu.
Nyumba hiyo inasemekana kuwa na na vyumba takribani vitano vya kulala lakini pia ikiwa na vitu vyote muhimu vinavyotakiwa kuwepo kwenye nyumba ya mcheza mpira ambaye anastehili kuitwa milionea.
of
Burudani inahusika pia ndani ya njengo huo
sehemu ya bwawa la kuogelea lililopo kwenye nyumba hiyo ambapo muogaji huoga kwa mvuke (Sauna)
.
Sehemu maalum ya kuhifadhia mvinyo (Wine cellar).
sehemu ya kupatia maakuli
Post a Comment