0
Dunga names Brazil squad
Dodo na Mario Fernandes ndio sura pekee mpya zilizomo kwenye kikosi cha Selecao kilichotajwa na kocha Carlos Dunga kinachojiandaa na michezo dhidi ya Argentina na Japan.

Dunga ametaja majina 22 watakaokuwemo kwenye ziara ya timu ya taifa ya Brazil ijulikanayo kama Gillette Brasil Global Tour mnamo mwezi wa October.

Mabingwa hao mara tano wa Dunia watakutana na Argentina kwenye mchezo ujulikanao kama Gillette Superclasico ya America mjini Beijing hapo October 11 kabla ya kuelekea Singapore ambako watakipiga dhidi ya timu ya taifa ya Japan hapo October 14.

Katika kikosi cha Dunga ziko sura mbili tu ngeni ambazo zinajiandaa kwaajili ya ya mchezo wa kirafiki mnamo mwezi wa October nazoni mlinzi wa klabu ya Inter Milan ya nchini Italy Dodo na mchezaji mlinzi wa  CSKA Moscow Mario Fernandes ambao wanakwenda kuchukua nafasi za mlinzi wa Real Madrid  Marcelo na Maicon wa AS Roma.

Kikosi kamili ni:-

Walinda Mlango: Jefferson (Botafogo), Rafael Cabral (Napoli).

Walinzi: David Luiz (Paris Saint-Germain), Marquinhos (Paris Saint-Germain), Gil (Corinthians), Miranda (Atletico Madrid), Dodo (Internacional), Filipe Luis (Chelsea), Mario Fernandes (CSKA), Danilo (FC Porto).

Viungo: Luiz Gustavo (Wolfsburg), Elias (Corinthians), Fernandinho (Manchester City), Ramires (Chelsea), Willian (Chelsea), Everton Ribeiro (Cruzeiro), Oscar (Chelsea), Coutinho (Liverpool).

Washambuliaji: Ricardo Goulart (Cruzeiro), Robinho (Santos), Neymar (Barcelona), Diego Tardelli (Atletico MG)

Post a Comment

 
Top