Liverpool imewashiwa taa ya kijani kuendelea na dili lake la kuufanyia upanuzi uwanja wa Anfield mnamo mwaka 2016 mara baada ya mamlaka ya jji la Liverpool kuridhia maombi yao.
Mtandao huu sasa unakuletea mambo saba muhimu unayohitaji kuyafahamu kuhusiana na upanuzi huo.
1. Upanuzi utachukua awamu mbili, awamu ya kwanza ni kuuongeza uwanja kutokea uwezo wa kuchukua watu 45,522 mpaka 54,000, na awamu ya pili ni kufikisha watu 58,000.
2. Awamu ya kwanza itajumuisha uongezaji wa viti kwenye eneo la lajukwaa kuu ambapo jumla ya viti 8,500 vitaongezwa kabla ya awamu ya pili ambapo jumla ya viti 4,800 vitaongezwa kwenye eneo la mzunguko.
3. Liverpool inatarajia kuanza kazi ya ujenzi wa upanuzi wa uwanja huo mnamo mwezi wa August 2016,na itawachukua jumla ya miezi 20 kukamilisha mradi huo.
4. Upanuzi huu hautakua tu na manufaa ya kuongeza watazamaji tu bali pia utatoa ajira za kudumu za nyongeza kwa takribani watu 40 lakini takribani watu 500 watatumika katika shughuli za ujenzi.
5. Upanuzi wa eneo la jukwaa kuu utakapokamilika basi jukwaa hiloa klabu ya Liverpool ndio litakua jukwaa lenye uwezo wa kuchukua atu wengi zaidi kuliko viwanja vyote nchini Uingereza.
6. Upanuzi pia utahusisha eneo la kumbukumbu la wahanga wa Hillsborough ambalo linaitwa ‘The Garden’.
7. Wakazi wa eneo la Liverpool watapewa ruhusa ya kutoa msaada wa kuongoza magari siku zote za michezo mbalimbaliitakayokuwa inafanyika katika dimba la Anfield.
Post a Comment