Mashabiki wa klabu ya Manchester United wanatarajia kukirudia kilekile walichokifanya dhidi ya kocha waliyetimuliwa ndani ya kikosi hicho David Moyes walipoamua kumpitishia ndege ndogo kwenye dimba la Old Traford ikiwa na bango lililokua likisomeka Get out Moyes safari hii wakitaka kupitisha bango hilo kwenye dimba la Santiago Bernabeu likimkaribisha mchezaji wao wa zamani Cristiano Ronaldo nyumbani Old Trafford.
Mshambuliaji huyo wa klabu ya Real Madrid aliondoka ndani ya klabu ya Manchester United mnamo mwaka 2009 mara baada ya misimu kadhaa ya mafanikio akiwa na mashetani wekundu hao wa kutoka jiji la Manchester katika majira ya joto yajayo.
Mashabiki hao wa klabu ya Manchester United wamechachanga pesa takribani paundi 3,000 kwaajili ya malipo ya ndege hiyo ili iweze kuruka siku ambayo klabu ya Real Madrid itakapokuwa ikikipiga dhidi ya nyambizi ya Villarreal siku ya jumaapili na bango hilo litakua limeandikwa ujumbe ‘Come home Ronaldo’ yaani rudi nyumbani Ronaldo.
Mwanzilishi wa kundi hilo la mashabiki wa klabu ya Manchester United anayefahamika kwa jina la Oli Grandidge, amesema: ‘Tuna mashabiki wenye nguvu sana na mshaikamano katika mabara yote Duniani na sote tumeunganishwa na kitu kimoja tu nacho ni Manchester United na upendo wetu kwa Cristiano akiwa kama mchezaji na mwanaadamu.
‘Hatuta simama mpaka tutakapo hakikisha kuwa Ronaldo amerejea United ambako ni kama nyumbani kwake.
‘Wanachama wa kundi hili duniani kote wamecagia pesa zao binafsi na rasilimali mbali mbali ili kuliwezesha tukio hili la kihistoria linalotarajia kufanyika ambapo bango litaapitishwa na ndege kuwasilisha ujumbe wetu kwa Ronaldo na Dunia kwa ujumla.
Post a Comment