0
Liverpool ALREADY working on deal to sign Benzema
Liverpool imeweka hadharani nia yake ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid Karim Benzema kwenye usajili wa mwezi January mwakani.

Taarifa zinadai kuawa Liverpool walikua wakifuatilia mwenendo ka Benzema tangu miaka miwili iliyopita na sasa taarifa kutoka nchini Uhispania zinadai kuwa meneja Brendan Rodgers anajiandaa kuweka ofa mezani kwaajili ya kumnasa mfaransa huyo.

Liverpool wamejulishwa kuwa mshambuliaji huyo hana furaha ndani ya klabu ya Real Madrid kwa sasa na hivyo yuko tayari kuelekea kwenye timu yoyote ile itakayo peleka ofa yenye maslahi kwa upande wake na klabu pia.

Inasemekana kuwa klabu ya PSG ya nhini Ufaransa itakua moja kati ya washindani wakubwa wa klabu ya Liverpool katika kuhakikisha wanazipata huduma za mshambuliaji huyo lakini Liverpool wanaonekana kuwa mstari wa mbele kuwa na uwezekano wa kumnasa mshambuliaji huyo.


Post a Comment

 
Top