Cristiano Ronaldo amerejea tena njiani msimu huu mara baada ya kutokuwa na msimu wa kuvutia sana mwaka jana kutokana na kuandamwa na mamivu aliyoyapata mnamo mwezi september mwaka jana.
Magoli yake matatu aliyoyafunga kwenye mchezo dhidi ya Deportivo La Coruna siku ya jumamosi yaliyoisaidia klabu yake ya Real Madrid kupata ushindi wa jumla ya magoli 8-2 yamemfanya afikishe idadi ya hat-trick 24 na hivyo kumfanya ashike nafasi ya pili nyuma ya Alfredo Di Stefano aliyefunga hat-trick takribani 28 huku akimpita Ferenc Puskas aliyefunga hat-trick 23.
Hat-trick hiyo inamfanya pia Ronaldo ashike nafasi ya pili katika orodha ya wachezaji waliowahi kufunga magoli matatu kwenye michezo ya La Liga ambapo Di Stefano aniishikiria na nafasi ya pili ikienda kwa ligendari wa klabu ya Athletic Bilbao Telmo Zarra aliyefunga hat-trick 22, wakati mchezaji wa zamani wa Dunia anayekipiga ndani ya klabu ya Barcelona Leonel Messi akiwa amekwishafunga mara 19.
Kwenye michuano ya Uefa Champions League Ronaldo alivunja rekodi ya kufunga takribani magoli 17 alipoisaidia klabu yake hiyo kuandikisha rekodi ya La Decima kwenye msimu wa 2013-2014 akiivunja ile ya mara 14 iliyowekwa na Lionel Messi, na goli lake la juzi alilolifunga dhidi ya klabu ya Fc Basel lilikua ni goli la 68 kwenye michuano ya Ulaya ikiwa ni magoli matatu pungufu ya mfungaji anayeshikiria rekodi ya kufunga magoli mengi kwenye michuano hiyo Raul Gonzalez Blanco mwenye magoli 71.
Post a Comment