Bastian
Schweinsteiger ametajwa kuwa ndiye nahodha mpya wa timu ya taifa ya Ujerumani akichukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa nahodha wa timu hiyo aliyeamua kuachana na soka la kimataifa Philipp Lahm.
Schweinsteige ataikosa michezo miwili ya timu yake ya taifa kutokana na kuwa na maumivu ya kifundo cha mguu ametajwa na kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani Joachim Loew ambaye pia amemteuwa kocha wa zamani wa klabu ya VfB Stuttgart, Thomas Schneider kuwa msaidizi wake katika benchi la Ufundi.
Schneider
anachukua nafasi ya aliyekuwa msaidizi wa Leow, Hansi Flick, ambaye amepanda cheo na kumlazimu kuiacha nafasi hiyo aliyoanza kuitumikia tangu mwaka 2006 kwani sasa amekuwa mkurugenzi wa ufundi wa chama cha soka cha nchini Ujerumani.
Ujerumani wanatarajiwa kukumbushia mchezo wa fainali ya kombe la Dunia kule nchini Brazil dhidi ya Argentina usiku huu kabla ya kucheza mchezo wa kufuzu kwaajili ya michuano ya Ulaya ya mwaka 2016 dhidi ya Scotland.
Low
atalazimika kufanya mabadiliko kadhaa kwenye kikosi chake cha kwanza kutokana na kujiuzuru kwa mshambuliaji Miroslav
Klose, nahodha wake wa zamani Lahm na mlinzi wake wa kati anayekipiga kwenye klabu ya Arsenal Per Mertesacker.
Post a Comment