Kocha wa mwaka duniani, Joachim Leow alihudu kwa miaka akijaribu
kuondoa shauku ya uwezo wake kabla ya kufanikiwa kwa bashasha ya
kuongoza taifa lake Ujerumani kunyakua ubingwa wa Kombe la Dunia.
Kabla ya dimba la Brazil ambalo liliadhimisha miaka minane kama
kinara wa kikosi almaarufu Die Mannschaft, Leow alinusa utukufu bila
kutamba kufuatia kufuzu semi fainali moja ya Kombe la Dunia, fainali ya
shindano la Ulaya na semi fainali ya Euro 2012.
Lakini vijana wake walisiaga wapinzani wao haswa katika adhabu kali
waliowapokeza wenyeji Brazil walipowazaba magoli saba kwa moja kwenye
mechi ya kihistoria kabla ya kuwazima Argentina 1-0 kwenye fainali
kusimama kileleni mwa mchezo wa kandanda.
“Kushinda Kombe la Dunia kulikuwa ni keki na taji hili limenogesha
ufanisi huo,” Leow alisema jijini Zurich baada ya kutwikwa taji hilo
mbele ya waalimu sugu Diego Simeone wa mabingwa wa Uhispania, Atletico
Madrid na Carlo Ancelotti wa mabingwa wa Ulaya, Real Madrid.
Msaidizi huyo wa zamani wa kocha Jurgen Klismann amesifiwa na vigogo
wastaafu Pele na Diego Maradona kwa kuleta mchezo wa mashambulizi
makali katika kikosi chake.
Sura yake ni mashuhuri Ujerumani ambapo anaongoza kampeni ya
matangazo ya biashara ya manukato lakini ni nadra kwa kocha huyo
kujitokeza hadharani kupitia vymbo vya habari.
Leow alikiri kabla ya dimba la dunia “saa inagonga” kwa muda wake
kama kinara lakini shirikisho la kandanda la nchi yake, DFB, walionesha
imani na uhodari wake kwa kumwongezea kandarasi hadi Kombe la Ulaya la
2016.
Post a Comment