Klabu za Manchester City na Swansea City zimefikia muafaka wa kuuziana mchezaji Wilfried Bonny kwa ada inayotajwa kufikia paundi milioni 30.
Kwa mujibu wa gazeti la The Mirror la nchini Uingereza limeandika kuwa vilabu hivyo viwili tayari vimekwisha kubaliana kwenye mambo ya msingi kuhusiana na mauzo ya mchezaji huyo na kinachosubiriwa sasa ni makubaliano binafsi tu baina ya Man City na Bonny.
Taarifa zinadai kuwamchezaji huyo raia wa Ivory Coast anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka minne ambao atakua akijikusanyia kiasi cha paundi 100,000 kwa wiki kama mshahara wake mara baada ya kuvuja jasho klabuni hapo.
Ikumbukwe tayari mchezaji huyo alisha waalifu mabosi wa klabu yake hiyo kuwa anataka kucheza ligi ya mabingwa barani Ulaya na hivyo itakapotokea kuwa kuna timu inayoshirki michuano hiyo basi ofa hiyo ifikiriwe zaidi.
Post a Comment