Mabosi wa klabu ya Liverpool wamesafiri kwenda nchini Ufaransa kwa minajiri ya kwenda kuwapigia magoti mabosi wenzao wa klabu ya Lille ili wauvunje mkataba wa mkopo wa muda mrefu wa mcshambuliaji mwenye asli ya nchini Kenya Divock Origi.
Liverpool ilimsainisha mshambuliaji huyo raia wa Ubeligiji kwa ada inayokisiwa kufikia kiasi cha paundi milioni 10 majira ya joto yaliyopita mara baada ya kuisha kwa michuano ya kombe la Dunia kwa makubaliano kuwa mara baada ya usajili huo atatakiwa kubakia kwa mkopo wa muda mrefu kwenye klabu ya Lille Metropolle.
Kwa sasa meneja Brendan Rodgers amejikuta akihitaji mno mshambuliaji wa kalba ya Origi ili kuongeza nguvu kwenye sehemu ya ushambuliaji wa klabu hiyo inayoonekana kuto kuwa na mwenendo mzuri kwa sasa.
Taarifa zinadai kuwa klabu ya Liverpool iko tayari kutoa hadi kiasi cha paundi milioni 3 ili waweze kuwashawishi mabosi wa Lille waweze kumuachia Origi ikiwa ni miezi 6 kabla ya kuisha kwa mkataba wake wa sasa wa mkopo.

Post a Comment