Theo Walcott alifurahia
sana kurudi kucheza soka tena Arsenal alipowachezea wakati wa ushindi
wao wa raundi ya tatu Kombe la FA Jumapili na kusema alifurahia pia
kucheza na “mchezaji wa kipekee” Alexis Sanchez.
Walcott alicheza dakika 76 wakati wa ushindi wa Arsenal wa 2-0 dhidi
ya Hull City uwanjani Emirates, ikiwa mara yake ya kwanza kuanza mechi
mwaka mmoja tangu aumie goti, jeraha lililomuweka nje ya Kombe la Dunia.
Alikuwa mnyamavu ingawa alionyesha matumaini uwanjani na mchezaji
huyo wa miaka 25 aliambia BBC: “Ilikuwa furaha kwangu binafsi kujitoa
kutu baada ya kukaa nje mwaka mmoja. Ilikuwa vyema sana kuhusika na
kupata nafasi kadha. Nilitaka kufunga lakini sikufanikiwa.”
Hata hivyo, kijana huyo anayesema anajizatiti kumaliza uchezaji wake
kama “jagina Arsenal” alieleza kuwa anashuku huenda anamtazama jagina
mwingine – Sanchez – aliyeng’aa mechi yote kabla ya kufunga bao la pili
la Arsenal dakika ya 82.
"Alexis Sanchez ni mchezaji wa kipekee na ilikuwa furaha kuwa naye uwanjani hatimaye.
Nasubiri
kucheza naye zaidi,” akasema Walcott.
Kurudi kwake ni habari njema kwa Uingereza pamoja na Arsenal, mabingwa
watetezi wa Kombe la FA, wanaopania kuimarisha nafasi yao ligini kipindi
cha pili cha msimu baada ya kushuka hadi nambari sita Ligi ya Premia.
Walcott alisema anahisi vyema sana kurudi kucheza baada ya upweke aliokumbana nao akijaribu kujiweka sawa kucheza.
“Nafikiri kiakili ni vigumu sana unapokuwa chumba cha matibabu peke
yako, wachezaji wenzako wanapotoka kwenda kufanya mazoezi au kucheza
Kombe la Dunia,” akasema mchezaji huyo, aliyeumia kano za goti.
"Lakini nilikuwa na mengi sana yaliyokuwa yakijiri nje ya uwanja maishani mwangu na hayo yalinisukuma.”
Walcott alionyesha hajapoteza kasi yake lakini kumalizia kwake, kwani
alipoteza nafasi moja wazi, kulionekana kuwa na kutu kiasi.
Chanzo,
Post a Comment