Nahodha wa Arsenal Mikel Arteta atakaa nje miezi mitatu baada ya
kufanyiwa upasuaji kifundo chake cha mguu wa kushoto ambacho kimemuweka
nje tangu mwishoni mwa Novemba, klabu hiyo ilisema Alhamisi.
Arsenal watakuwa pia bila difenda wa kimataifa wa Ufaransa Mathieu
Debuchy hadi Aprili baada yake kupasuliwa bega aliloumia akicheza dhidi
ya Stoke City wikendi iliyopita.
Arteta,a mbaye ni kiungo wa kati wa Uhispania, alitolewa kijifupa na
kwenye tovuti yao (www.arsenal.com), Arsenal walisema: "Upasuaji
ulifanyika vyema na Mikel sasa ataponya jeraha kwa kipindi
kinachotarajiwa kuwa miezi mitatu.”
Meneja Arsene Wenger aliongeza: "Mikel amefanyiwa upasuaji na kila
kitu kiliendelea vyema. Alikuwa akishindwa kutembela kutokana na tatizo
kifundo chake cha mguu na alikuwa akifura na kuathirika misuli ya sehemu
ya chini ya mguu.
“Hili lilitulazimu kuamua afanyiwe upasuaji na ni suluhisho njema
linalompa nafasi bora zaidi ya kupona kabisa.”
Hajacheza tangu atolewe uwanjani dakika ya 67 Arsenal walipolaza
Borussia Dortmund 2-0 Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya uwanjani Emirates
Novemba 26.
Wenger aliongeza kuwa Debuchy, 29, pia alifanyiwa upasuaji bega lake la kulia baada yake kuumia.
“Ni jambo la kusikitisha sana kwa Mathieu, ni huzuni kwani amefanyiwa upasuaji mara mbili msimu mmoja.
“Amerudi juzi tu, alicheza mechi saba na sasa yuko nje tena.
Ninahesabu miezi mitatu kwa Mathieu kwa sababu itakuwa tatizo kuguswa
begani.”
Debuchy alianza mechi saba za kwanza za Arsenal msimu huu pamoja na
ushindi wao Community Shield dhidi ya Manchester City uwanjani Wembley
na kisha akakosa miezi mitatu baada ya kuumia kifundo cha mguu dhidi ya
City Septemba 13.
Alirudi kucheza mechi ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya
Galatasaray Desemba 9 na akahifadhi nafasi yake kikosini hadi pigo la
majuzi lililotokea alipogongana na Marko Arnautovic wa Stoke na
kuangukia mabango ya matangazo.
Post a Comment