Simba
sasa imeamka kwenye Kombe la Mapinduzi baada ya kufanikiwa kutinga nusu
fainai ya michuano ya Kombe la Mapinduzi kwa kuichabanga Taifa ya Jang'ombe kwa mabao 4-0.
Simba
imeonyesha inaweza baada ya kuzitumia dakika 45 za kipindi cha pili kwa
kuichapa Taifa mabao yote manne kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Shujaa
wa Simba leo ni Ibrahim Ajib aliyefunga mabao matatu, hat trick na
kufanikiwa kuondoka na mpira wa zawadi wakati mkongwe Shabani Kisiga
alimalizia bao la nne.
Simba
ilitawala mpira tokea kipindi cha kwanza, lakini Taifa walitoa upinzani
mkubwa na kufanya wamalize mpira wakiwa sare ya bila bao hadi mwisho wa
kipindi cha kwanza.
Nyota wa mchezo huo alikuwa ni beki mpya wa Simba, Ramadhani Kessy ambaye aliondoka na zawadi ya king'amuzi ya king'amuzi.
Post a Comment