Tuzo ya mchezaji Bora wa dunia wa
Fifa kwa mwaka 2014 inatarajiwa kutangazwa leo ambapo tayari wachezaji
watatu wamechujwa ili kuania tuzo hiyo inayojulikana kwa jina la FIFA
Ballon d'Or 2014.
Wachezaji watatu waliobaki
kwenye fainali ni pamoja na Christiano Ronaldo ambaye ni mchezaji wa
timu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno.
Mwingine ni Lionel Messi mshambuliaji wa Barcelona na mchezaji wa timu ya taifa ya Argentina.
Na wa tatu ni Manuel Neuer Mlinda mlango wa Bayern Munich ambaye pia hudakia timu yake ya taifa ya Ujerumani.
Post a Comment